“Nimeumia sana”, huu ni ujumbe uliochapishwa na afisa habari wa klabu ya Yanga Sc Ali Kamwe ikiwa ni dakika chache mara baada ya kumalizika kwa mchezo wa NMB Mapinduzi Cup ambao uliwakutanisha Simba Sc dhidi ya Azam Fc.
Simba Sc walikuwa wenyeji kwenye mchezo huo ambao umemalizika kwa Azam and kupata ushindi mwembamba wa goli moja kwa sifuri na ushindi huo umewapa nafasi ya kwenda katika hatua ya fainali ya michuano hii msimu huu.
Mara baada ya kumalizika kwa mchezo huo, Ali Kamwe kupitia kwenye ukurasa wake wa Instagram amechapisha taarifa fupi ya picha mjongeo inayomuonyesha akiwa kama analia mara baada ya kuona Simba Sc wanaondolewa kwenye michuano hiyo.
Ali Kamwe pengine alikuwa anatamani kuona Simba Sc wanashinda kwenye mchezo wa leo ili atengeneze mazingira ya kwenda kucheza nao mchezo wa fainali ya michuano hii lakini mambo yamekuwa tofauti kwani mnyama ameondolewa kwenye hatua hii ya nusu fainali.
Ali Kamwe alikuwa anatamani kuona wanakutana na Simba Sc kwenye mchezo wa fainali kutokana na ukweli kwamba Yanga Sc wamekua na uhakika wa kupata matokeo chanya kwenye mechi ambazo wanakutana na Simba Sc pengine kuliko timu zingine.
Rekodi ya Simba Sc kufungwa mara kwa mara na Yanga Sc ndio sababu pekee inayomfanya Ali Kamwe na baadhi ya mashabiki wa klabu ya Yanga Sc kufurahia zaidi mechi ambazo timu yao inakuwa inacheza dhidi ya Simba Sc pengine kuliko timu nyingine yoyote ile ambayo inashiriki Nbc Premier league.
Yanga Sc wakishinda kwenye mchezo wao wa kesho ambao watacheza dhidi ya Singida Black Stars basi watakutana na kibarua cha kucheza mechi ya fainali dhidi ya Azam Fc.
