
Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba SC, Ahmed Ally {@ahmedally_}, ameendeleza kutoa maoni yake ya kijasiri baada ya mchezo wa dabi ya Kariakoo, safari hii akimulika usajili wa wapinzani wao. Kupitia ukurasa wake wa kijamii, Ahmed Ally ametoa tathmini yake kuhusu uwezo wa mchezaji mpya wa Yanga, Okelo, akimlinganisha na winga wa klabu hiyo Denis Nkane waliyemtoa kwa mkopo.
Katika andiko lake, Ahmed Ally {@ahmedally_} ameeleza:
”Nimemuangalia yule Okelo vizuri hana anachomzidi Denis Nkane labda English tuu”.
