Serikali imesema hakuna mtego wowote uliowekwa kwa Askofu Dkt. Josephat Gwajima, unaotokana na kufunguliwa kwa Kanisa la Ufufuo na Uzima analoliongoza
Kauli hiyo ya serikali imetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Dar es Salaam Wakili Albert Msando kwaniaba ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi George Simbachawene alipofika Kanisani hapo leo, Jumanne Novemba 25.2025, ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa maelekezo ya Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba aliyotoa Novemba 24 mwaka huu yaliyotaka kufunguliwa kwa Kanisa hilo ili waumini wake waendelee kufanya ibada huku likiwa kwenye uangalizi maalum
Wakili Msando amelazimika kutoa ufafanuzi huo kutokana na taarifa zilizoenea kwenye mitandao ya kujamii kuwa huenda kufunguliwa huko ni sehemu ya mtego wa kutaka kumkamata Askofu Dkt. Josephat Gwajima
Aidha, Wakili Msando amewaelekeza viongozi wa Kanisa hilo kufanya ukaguzi na kufanya ulinganifu tangu walivyoondoka Kanisani hapo hadi sasa, na kama wataona kuna kasoro yoyote wasisite kwenda Ofisini kwake kumpatia taarifa.

