Alex Ngereza ‘Mlikosea Sana Kumfananisha Chama na Pacome’

“Mlikosea sana kumfananisha Pacome Zouzou na Chama kipindi kile na kizuri nilibaki na msimamo wangu kwamba Pacome sio level za Chama na hafiki hata kidogo mkanibishia bila sababu za msingi

Niliwambia tangu mwanzoni kwamba Pacome hajawahi kuwa mchezaji tishio ila amekuwa tishio kwetu na baada ya kupewa hype kubwa na wengine walilipwa ili wamsifiie hata akifanya kitu kidogo ndio maana alikuwa anapewa sifa hata kwenye vitu vidogo vidogo

Simaanishi kwamba ni mchezaji mbaya,HAPANA,bali tulimpa ukubwa ambao alikuwa hastahili kuupewa, nasikia Yanga wanataka kuachana nae ni sawa ila wakati huo mnipe na mimi pongezi kwasababu yote ambayo nilisema kuhusu yeye ndio yanaonekana

Nilisema kuhusu majeraha ya mara kwa mara ✓
Nilisema kuhusu kupoteza mipira kirahisi ✓
Nilisema Pacome ana kiwango cha kawaida ni ngumu kudumu Yanga kwa miaka minne ✓

Ongezeni na kingine ambacho mnakumbuka nilisema kuhusu Pacome 😀

Ameandika mchambuzi ALEX NGEREZA.!

Related Posts