AMEANDIKA ✍️ @alikamwe
We Love You @djiguidiarraofficial
Nimefurahi sana Leo mchana wakati Tukiwasili Airport hapa Algers, Rais wa Klabu ya @yangasc ENG. HERSI SAID akimpokea Begi mchezaji wake, Diarra aliyekuwa akitembea kwa kuchechemea
Ndio, djiguidiarraofficial jana alipata jeraha la enka kipindi cha kwanza, akiwa Dressing Room wakati wa mapumziko, mguu wake ulianza kuvimba na kila mmoja aliamini asingeweza kuendelea
Tayari Kocha wa Makipa alishatoka uwanjani na @_mshery kwa ajili ya Warm Up ili Sub ifanyike..
Lakini katika hali isiyotarajiwa na wengi, djiguidiarraofficial aliwaomba madaktari kupambana na mguu wake kupunguza uvimbe ule kisha akapigwa bandej za kutosha na Mwamba akavaa kiatu na kumwambia Kocha.. NAWEZA KURUDI UWANJANI
Maumivu ni makali mguuni Lakini @djiguidiarraofficial alitaka kurudi uwanjani kuipambania Nembo ya YOUNG AFRICANS SPORTS CLUB
Hakuna aliyeamini.. @djiguidiarraofficial akarudi uwanjani na KUFANYA SAVE KALI ZA MCHEZO akiwa na Maumivu Makali sana mguuni..H
What A Warrior
Huyu ni zaidi ya mpambanaji, ni zaidi ya Mwanachama.. Ni zaidi ya Binadamu wa kawaida anapokuwa na jezi ya @yangasc uwanjani
@djiguidiarraofficial anaipenda Yanga na Yuko tayari kwa Lolote …
TOP PROFFESIONAL🧤

