
Aliyekuwa Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Amos Makalla ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha.
Uteuzi huo wa Makalla ni sawa na kupishana ‘viti’ na Kenani Kihongosi ambaye alikuwa mkuu wa mkoa huo na kwa sasa ameteuliwa kushika wadhifa ulioachwa wazi na Makalla kwenye Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Kwa mujibu wa taarifa ya Ikulu iliyosainiwa na Naibu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Shaaban Kissu, Makalla ataapishwa Agosti 26, 2025 Ikulu ya Chamwino, Dodoma.

