
UHISPANIA: Timu ya FC Barcelona imefanikiwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Uhispania (#LaLiga) kwa staili ya kumchakaza mpinzani wake wa jadi, #RealMadrid kwa magoli 2-0 kwenye Uwanja wa Camp Nou.
Ushindi huo unaifanya Barcelona kufikisha pointi 91 ikimaanisha hakuna timu inayoweza kufikisha alama hizo, Real Madrid ipo nafasi ya pili ikiwa na pointi 77, timu zote zikiwa zimesaliwa na michezo mitatu kabla ya kukamilisha msimu wa 2025/26 katika ligi hiyo.
