
BASATA Yawashusha Rungu Harmonize, Nandy, Sanga na Waandaaji wa Matukio
Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limewatoza faini na kuwachukulia hatua za kinidhamu wasanii mashuhuri nchini pamoja na makampuni ya uandaaji wa matukio baada ya kubainika kukiuka kanuni na maadili ya kazi za sanaa nchini Tanzania.
Miongoni mwa walioathirika na maamuzi hayo ni pamoja na wasanii Rajab Abdulkahali (Harmonize), Faustina Charles Mfinanga (Nandy), mwongoza video Kennedy David Sanga, pamoja na makampuni ya uandaaji wa mashindano ya urembo.
Summary ya Maamuzi na Adhabu Zilizotolewa:
1. Harmonize (Rajab Abdulkahali)
-
Kosa: Kusambaza video ya wimbo “Kudos” inayokiuka maadili ya Kitanzania na kuvunja heshima ya mtazamaji (Kanuni ya 20(a)).
-
Adhabu:
-
Kuondoa mara moja video hiyo kwenye mitandao yake ya kijamii.
-
Kulipa faini ya TSh 5,000,000 ndani ya siku 14.
-
Kufungiwa kujishughulisha na kazi za sanaa hadi atakapotekeleza maagizo yote.
-
2. Kennedy David Sanga (Director wa Video)
-
Kosa: Kuongoza na kuandaa video ya wimbo “Kudos” isiyozingatia maadili.
-
Adhabu:
-
Kufuta video hiyo kwenye mitandao yake.
-
Kulipa faini ya TSh 5,000,000 ndani ya siku 14.
-
Kufungiwa kufanya kazi za sanaa hadi atakapokamilisha masharti ya adhabu.
-
3. Avil Contractors Company Ltd (Waandaaji wa Miss Grand Tanzania)
-
Kosa: Kuendesha shindano la Miss Grand Tanzania bila kuwa na kibali rasmi cha tukio kutoka BASATA.
-
Adhabu:
-
Kulipa faini ya TSh 3,000,000 ndani ya siku 14.
-
Kusitishwa kujishughulisha na matukio ya sanaa hadi faini hiyo itakapolipwa.
-
4. Nandy (Faustina Charles Mfinanga)
-
Kosa: Kuvaa vazi lisilo na staha linalokiuka maadili wakati akitumbuiza kwenye fainali za Miss Universe Tanzania 2026.
-
Hatua Zilizochukuliwa: Msanii huyo amekiri kosa, ameondoa video hiyo mitandaoni na tayari amelipa faini ya TSh 3,000,000. Ameruhusiwa kuendelea na shughuli zake za sanaa chini ya uangalizi maalum.
5. Millen Prive & Co. Lifestyle Limited (Waandaaji wa Miss Universe Tanzania)
-
Kosa: Kuruhusu ukiukaji wa maadili ya mavazi jukwaani wakati wa tamasha lao.
-
Adhabu:
-
Kulipa faini ya TSh 3,000,000 ndani ya siku 14.
-
Kupewa onyo kali la kutojirudia kwa kosa hilo katika matukio yajayo.
-
BASATA imewakumbusha wasanii na waandaaji wote wa kazi za sanaa nchini kuhakikisha wanafuata sheria, kanuni na maadili ya Kitanzania ili kuepuka hatua kali za kisheria na kijamii.
