BREAKING: Murtaza Mangungu Akosa Sifa za Awali Kuwania Uenyekiti Simba SC, Wanne Wapita

BREAKING: Murtaza Mangungu Akosa Sifa za Awali Kuwania Uenyekiti Simba SC, Wanne Wapita
BREAKING: Murtaza Mangungu Akosa Sifa za Awali Kuwania Uenyekiti Simba SC, Wanne Wapita

Murtaza Mangungu Akosa Sifa za Awali Kuwania Uenyekiti Simba SC, Majina Manne Yapitishwa

Dar es Salaam – Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imetoa orodha ya awali ya wagombea waliopita katika mchujo wa kwanza kuwania nafasi mbalimbali za uongozi kwenye Uchaguzi Mkuu wa Klabu ya Simba SC, huku jina la Mwenyekiti wa sasa, Murtaza Ally Mangungu, likikosekana.
Katika orodha hiyo ya awali iliyotolewa na kamati hiyo, jumla ya wagombea wanne (4) pekee ndio waliopitishwa kuwania kiti cha juu cha Mwenyekiti wa klabu hiyo kati ya saba waliochukua na kurejesha fomu hapo awali.

Wagombea Waliopitishwa Nafasi ya Mwenyekiti (4)

Kwa mujibu wa tangazo hilo la Kamati ya Uchaguzi ya TFF, majina yaliyopita katika hatua hii ya awali kuwania uenyekiti wa Wekundu wa Msimbazi ni:
  1. Anindum Jonas Semu

  2. Geoffrey Irick Nyange

  3. Dkt. Seif Ramadhani Muba

  4. Swedy Khamis Mkwabi

Mwelekeo Mpya Kuelekea Uchaguzi Mkuu

Kutokuwepo kwa Murtaza Mangungu—ambaye alikuwa akitetea kiti chake—pamoja na wagombea wengine wawili walioenguliwa katika hatua hii, kunafungua ukurasa mpya na kuibua ushindani wa sura mpya katika kinyang’anyiro hicho cha uongozi ndani ya Simba SC.
Hata hivyo, kwa mujibu wa kanuni za uchaguzi, mchakato huu bado unaendelea na hatua za rufaa na pingamizi zinaweza kufuata kabla ya Kamati ya Uchaguzi ya TFF kutoa orodha ya mwisho ya wagombea watakaopigiwa kura katika Uchaguzi Mkuu wa klabu hiyo.

Related Posts