Shirikisho la Soka Afrika (CAF) limethibitisha kupokea malalamiko kutoka kwenye michezo miwili ya kundi B iliyopigwa November 28,2025
CAF imetoa taarifa kuwa inalaani vikali uvunjaji mkubwa wa usalama uliotokea wakati wa mechi ya Ligi ya Mabingwa ya TotalEnergies CAF iliyochezwa tarehe 28 Novemba 2025 kati ya ASFAR (Morocco) dhidi ya Al Ahly (Misri) na JS Kabylie (Algeria) dhidi ya Young Africans (Tanzania).
Aidha imeongeza kuwa matukio hayo yamewasilishwa rasmi kwenye Bodi ya Nidhamu ya CAF kwa ajili ya uchunguzi.

