
Kikao cha Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) taifa kimemteua Clayton Chiponda ‘Babalevo’ kuwa mgombea atakayepeperusha bendera ya chama hicho katika Jimbo la Kigoma Mjini mkoani Kigoma.
Hayo yamesemwa na Katibu wa Halmashauri Kuu (NEC), Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama cha Mapinduzi CPA Amos Makalla, akizungumza na wanahabari usiku wa Jumamosi Agosti 23, 2025 katika Makao Makuu ya CCM Dodoma.
