Celestine Ecua Mambo Fresh Aelekea zake JS Kabylie

Klabu ya JS Kabylie ya Algeria imekamilisha dili la kumsajili kiungo Celestin Ecua kutoka Yanga. 🚨✨

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Algeria, JS Kabylie ilikamilisha dili hilo kwa makubaliano ya mkopo, huku ikilenga kuimarisha kikosi chake katika kipindi hikic ha dirisha dogo.

Ecua, ambaye alisajiliwa Yanga mwanzoni mwa msimu huu, anatajwa kuvutiwa na changamoto mpya nje ya Tanzania, huku klabu hiyo ya Jangwani ikimpa nafasi hiyo ili apate uzoefu zaidi katika soka la ushindani wa juu barani Afrika.

Ecua anakuwa mchezaji mwingine kutoka Ligi Kuu Bara kujiunga na soka la Algeria, akitanguliwa na Jean Ahoua aliyeondoka Simba SC na kujiunga na CR Belouizdad wiki iliyopita.

Related Posts