Mchezaji kinda na mwenye kiwango kizuri wa Timu ya Taifa ya Uganda Allan Okello amechochea tetesi za usajili wake baada ya kumfuata (kumfollow) rasmi Rais wa Yanga Engineer Hersi Said kwenye mtandao wa Instagram.
Mbali na hilo Okello pia amefollow ukurasa wa Klabu Yanga SC jambo linalozidi kuwapa mashabiki hisia kuwa kuna mazungumzo yanaendelea kati ya pande hizo mbili.
