
Rais wa Marekani Donald Trump amesema Marekani utawala wake utakomesha mambo ambayo yamekuwa yakifanywa na Iran hasa uzalishaji mpango wa kuzalisha silaha za nyuklia na mashambulizi ambayo wamekuwa wakifanya kwa karibu miaka 47, kwa kuishambulia Marekani na kuwaua Wamarekani.
Amesema Marekani inaangamiza uwezo wa makombora ya Iran na kuhakikisha wanaharibu uwezo wao wa kuzalisha makombora mapya.
Pamoja na hayo amesema tayari kwa kushirikiana na Israel Marekani imeangamiza angalau meli 10 ambazo wamezamisha. Akisisitiza kuwa mfadhili mkuu wa kigaidi duniani hatoweza kamwe kupata silaha za nyuklia
