Esther Matiko wa Chadema Atimkia Chama Cha Mapinduzi (CCM)
Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Tarime kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na baadaye Mbunge wa Viti Maalum Esther Nichoulas Matiko amethibitisha kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM) na anatarajiwa kuchukua fomu ya kukiomba chama chake hicho kipya kumpa ridhaa kuwania Ubunge wa Tarime Mjini kwa kipindi cha 2025-2030.
Matiko amekoleza joto la Ubunge wa Tarime Mjini ambapo anatarajia kumenyana na vigogo kadhaa akiwamo Mbunge anayemaliza muda wake Michael Kembaki.

