Freeman Mbowe Ahudhuria Uzinduzi Rasmi wa Bwawa la Umeme la Nyerere (JNHPP)

Aliyekuwa Mwenyekiti wa CHADEMA na Mbunge wa zamani wa Hai, Freeman Mbowe, ni miongoni mwa viongozi na wageni waalikwa waliohudhuria hafla ya uzinduzi rasmi wa Kituo cha Kuzalisha Umeme cha Julius Nyerere (JNHPP) kilichopo Wilayani Rufiji, Mkoa wa Pwani.

Mradi huo mkubwa wa kimkakati una uwezo wa kuzalisha Megawati 2,115 za umeme, hatua inayotajwa kuwa mkombozi mkubwa katika kuongeza nishati nchini na kuimarisha shughuli za kiuchumi na kijamii.

Ushiriki wa Mbowe katika hafla hiyo umevuta hisia za wengi, akiungana na viongozi mbalimbali wa kitaifa na wadau wa sekta ya nishati kushuhudia hatua hiyo ya kihistoria kwa taifa.

Related Posts