Gachi Amuomba Radhi Yammi Baada ya Kuzua Taharuki Mitandaoni

Gachi Amuomba Radhi Yammi Baada ya Kuzua Taharuki Mitandaoni
Gachi Amuomba Radhi Yammi Baada ya Kuzua Taharuki Mitandaoni

Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Fatma Omary maarufu kama Gachi
Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Fatma Omary maarufu kama Gachi, amejitokeza hadharani kumuomba radhi msanii mwenzake Yammi kufuatia tuhuma alizozitoa mitandaoni hivi karibuni akimtuhumu kumchukulia mwanaume wake.

Gachi aliambatana na wakili wake wakati wa kutoa tamko hilo, akisisitiza kuwa tuhuma alizotoa hazikuwa na maadili.

“Sikuwaza Kwa Kina” amesema Gachi

Kwa mujibu wa maelezo yake, Gachi alikiri kuwa aliongea kwa hasira na bila kutafakari athari zake, akiongeza kuwa kitendo hicho kimeleta taharuki na kuharibu taswira yake pamoja na kumuumiza mhusika aliyemtaja.

Msanii wa Bongo Fleva, Yammi
Alisema kuwa anajutia kwa dhati kauli hizo na yuko tayari kuchukua hatua zozote za kurekebisha makosa aliyoyafanya.

Mbali na kumuomba radhi Yammi, Gachi pia aliwaomba Watanzania kumsamehe, akieleza kuwa amejifunza umuhimu wa kujizuia na kuthibitisha taarifa kabla ya kuzitoa hadharani.

“Naomba radhi kwa wote niliowakwaza. Yale niliyoyaandika hayakuwa na maadili na hayakunionesha mimi halisi,” alinukuliwa akisema.

Related Posts