Mtendaji mkuu wa Manara Tv Haji Sunday Manara ameibuka na taarifa nzito sana mara baada ya klabu ya Simba Sc kupoteza ubingwa wa kombe la shirikisho barani Afrika ambao wamecheza shidi ya klabu ya RS Berkane kutoka nchini Morocco.
Simba Sc walikuwa wenyeji kwenye mchezo huo ambao umepigwa siku ya leo Jumapili tarehe 25 Mei, katika dimba la New Amaan Complex, mchezo huo umemalizika kwa sare ya kufungana 1_1.
Simba Sc wamepotez ubingwa ubingwa huo kwa matokeo ya jumla ya magoli matatu kwa moja, hii inatokana na matokeo ya mchezo wa awali ambao Simba Sc walipoteza kwa tofauti ya magoli mawili kwa sifuri.
Mara baada ya kupoteza mchezo huo, Haji Manara ameibuka na taarifa nzito ya kuwakejeli Simba Sc ambao wameshindwa kufanya maajabu ya kushinda taji hili kwenye mchezo wa leo ambao umepigwa kwenye ardhi ya Tanzania.
Haji Manara katika taarifa yake ameeleza wazi kufurahishwa sana na kitendo cha Simba Sc kupoteza mchezo huo kwa sababu endapo kama wangeshinda wangeleta kelele nyingi mtaani kwa watani wao wa jadi Yanga Sc ambao wao walitolewa mapema sana kwenye hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa barani Afrika.

Haji Manara amewai kufanya kazi ndani ya klabu ya Simba Sc, aliondoka ndani ya klabu hiyo kutokana na migogoro ambayo ilijitokeza baina yake na viongozi wakubwa wa klabu ya Simba Sc wakiongozwa na aliyekua mtendaji mkuu wa klabu hiyo mwanadada Barbra Gonzalez.
Mara baada ya Manara kuondoka ndani ya klabu ya Simba Sc, amekuwa na chuki binafsi na klabu hiyo kwani hatamani kuona ikipata mafanikio yoyote kwenye michuano ya ndani pamoja na ile ya kimataifa.
