
Mchezo ulizikutanisha Yanga Sc na Simba Sc timu hizo kongwe zenye historia ndefu katika soka la Tanzania, huku kila upande ukihitaji matokeo chanya kujiimarisha katika msimamo wa ligi.
Akizungumzia dabi hiyo, msemaji wa zamani wa klabu hizo, Haji Manara, amesema kuwa mashabiki hawapaswi kutoa hitimisho la kudumu kutokana na matokeo ya mchezo mmoja.
“Ni shabiki mwendawazimu tu atakayeamini kuwa Yanga wataendelea kuifunga Simba milele, jambo hilo halipo kwenye mpira wa miguu,” alisema Manara.
Aliongeza kuwa matokeo ya dabi hiyo hayapaswi kuchukuliwa kama mwisho wa ubora wa timu yoyote, kwani soka hubadilika kulingana na kiwango cha timu siku husika.
