
Mshambuliaji wa Liverpool na timu ya taifa ya Misri, Mohamed Salah, amefikia makubaliano na klabu hiyo ya kuondoka mwishoni mwa msimu huu.
Salah ameisaidia Liverpool kutwaa mataji mbalimbali ikiwemo Ligi Kuu Uingereza, UEFA Champions League, Kombe la Dunia la Klabu, UEFA Super Cup na FA Cup. Hadi sasa ameifungia klabu hiyo mabao 255 katika mechi 435, akishika nafasi ya tatu katika orodha ya wafungaji bora wa muda wote wa Liverpool.
