Msanii wa muziki wa kizazi kipya hitmaker wa “MIDA YA KAZI” na “NAUMIA ROHO” Abraham Kassembe maarufu kama “DULLAYO” muda mrefu amekuwa akionekana kwenye video mbalimbali mtandaoni akiwa katika hali isiyo nzuri kimuonekano nahata kiafya.
Hivi leo msanii huyo, ameonekana kuchukua hatua chanya za mabadiliko katika maisha yake, baada ya muda mrefu watu kujiribu kumshauri nakujaribu kumtaka akapate tiba za mihadarati kutoka nyumba spesho za tiba hizo kama (SOBER HOUSE)
Msanii wa muziki DULAYO ambaye anakabiliwa na uraibu wa pombe hali iliyofanya apoteze dira ya maisha, anamshukuru rapa @mrbluebyser1988 kwa kumchukua na kumpeleka katika kituo cha kuondoa uraibu wa pombe.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Pili wa Misana Foundation, Pili Misana amesema amekuwa akipigiwa mara kadhaa na rapa Blue kwaajili ya wasanii ambao wanapata matatizo.
“DULLAYO” ameelezea namna anavyojisikia kwasasa, naametoa shukran zake za dhati kwa wadau na mashabiki wake, hii ni habari njema kwa kiwanda cha Muziki wa bongo fleva, mara ya mwisho hatua kama hizi zilichukuliwa na msanii “CHID BENZ” ambae kwasasa anaendelea vyema namaisha yake.
