Na Ally Mandai.
Anaitwa Boubou Traore rekodi zinaonyesha mwamuzi huyo amechezesha mechi 25 za klabu Afrika, huku katika michezo hiyo wenyeji wameshinda 17, ilhali wageni wakishinda sita na mbili zikiisha kwa sare. Pia anasifika kwa kumwaga kadi kama njugu kwani kupitia mechi hizo ametoa za njano 86 na nne nyekundu kuonyesha kuwa hana utani uwanjani.
Na leo tumeona maamuzi yake dhidi ya Morocco vs Tanzania ni refa wa kugawa Kadi na nyingi zikienda Tanzania huku Morocco wakipewa moja tu.
Alipata beji ya FIFA mwaka 2014 na ndiye aliyekuwa mwamuzi wa mchezo kati ya Yanga SC 4-0 Belouzdad
