Huyu ndiye, Ayatollah Ali Khamenei Kiongozi Mkuu Iran

Huyu ndiye, Ayatollah Ali Khamenei Kiongozi Mkuu Iran
Huyu ndiye, Ayatollah Ali Khamenei Kiongozi Mkuu Iran

Ayatollah Ali Khamenei, 86, amekuwa kiongozi wa pili mkuu tangu mapinduzi ya 1979 baada ya kifo cha Ruhollah Khomeini mnamo mwaka 1989 na mwenye mamlaka ya juu zaidi nchini humo.

Kama kiongozi mkuu, alikuwa akidhibiti siasa za nchi, jeshi na taasisi za kidini za Iran ikiwa ni pamoja na kutoa mwongozo wa uhusiano wa masuala ya kigeni.

Kabla ya kuchukua wadhifa huo alikua rais wa taifa hilo kwa mihula miwili kuanzia 1981 hadi 1989.

Mamlaka ya ofisi yake yamemfanya Khamenei kuwa na nguvu zote kama mkuu wa nchi na kamanda mkuu wa jeshi, ikiwa ni pamoja na kikosi cha Revolutionary Guards.

MALEZI YA KIDINI

Ali Khamenei alizaliwa Mashhad, jiji la pili kwa ukubwa nchini Iran, mwaka wa 1939.

Baba yake alikuwa kiongozi wa kidini wa Shia, tawi kuu la Kiislamu la Iran.

Khamenei alizungumzia sana utoto wake kama “maskini lakini mcha Mungu”, akisema mara kwa mara hakula chochote ila “mkate na zabibu”.

Alianza masomo ya dini huko Mashhad, akakaa kwa muda mfupi huko Najaf, Iraqi, kisha akasoma katika chuo cha dini katika mji wa Qom nchini Iran.

Wanachuoni kadhaa walimfundisha, ikiwa ni pamoja na Khomeini, ambaye baadaye alianzisha Jamhuri ya Kiislamu.

Wakati wa mapinduzi, Khamenei hakuwa mtu maarufu kati ya watu waliokuwa karibu na Ayatollah Khomeini, lakini alijulikana haraka baada ya ghasia hizo.

Alijiunga na Baraza la Mapinduzi lililoongoza mapinduzi, na kuwa baraza la uongozi la muda baada ya kuanguka kwa utawala wa Shah.

Jukumu lake la kwanza la serikali ya Jamhuri ya Kiislamu lilikuwa naibu wa Wizara ya Ulinzi.

Khomeini alimteua kuwa kiongozi wa Sala ya Ijumaa huko Tehran mwaka huo, cheo ambacho alikishikilia rasmi kwa muda mrefu.

Mahubiri ya kisiasa ya Ali Khamenei, yaliyotangazwa nchi nzima, yalimfanya ajulikane ndani ya uongozi mpya.

Chanzo: BBC

Related Posts