
Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) imeliondoa jina la Mgombea Urais wa Tanzania kupitia Chama cha ACT-Wazalendo, Luhaga Mpina kwenye orodha ya wagombea wa Urais wa Tanzania mwaka 2025.
Kwa mujibu wa taarifa ya leo Septemba 15, 2025 iliyotolewa na Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Ndugu Kailima, R. K imeeleza kuwa INEC imefikia hatua hiyo baada ya kukubali pingamizi lililowasilishwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Hamza Johari dhidi ya uteuzi wa Mpina

