Nature

IRAN Hawacheki na Wowote, Walipiza Kisasi Kwa Marekani, Walipua Kituo Hichi Leo

Katika taarifa iliyotolewa Jumatatu, vyanzo vya kuaminika vimeripoti kuwa kituo cha kijeshi cha Marekani kilichopo katika jimbo la Hasakah, magharibi mwa Syria, kimelengwa na shambulio la makombora.

Kwa mujibu wa vyanzo hivyo, makombora ya kutengenezwa nchini Iran yalilenga kambi hiyo ya kijeshi ya Marekani iliyoko eneo la Al-Shadadi.

Hata hivyo, mifumo ya ulinzi ya anga ya Marekani ilifanikiwa kuyazuia makombora hayo kabla hayajaleta madhara yoyote.

Baada ya shambulio hilo, hatua kali za kiusalama ziliimarishwa katika lango kuu la kuingilia kambini humo, huku wanajeshi wa Marekani wakionekana kuchukua tahadhari zaidi ili kuhakikisha usalama wa eneo hilo unaendelea kudhibitiwa.

Mpaka sasa hakuna taarifa rasmi kuhusu majeruhi au uharibifu wowote uliosababishwa na shambulio hilo.

Tutaendelea kufuatilia taarifa zaidi kuhusu tukio hili.

MiddleEastCrisis

Related Posts

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *