Nature

Jamaa aandika jina la ex wake mwili mzima akisema hakubali kumpoteza tena

Wakaazi wa Mbezi Beach walishuhudia tukio lisilo la kawaida siku ya Jumatano, Julai 30, 2025, baada ya kijana mmoja kujichora jina la mpenzi wake wa zamani kwa mwili mzima akidai hawezi kuvumilia kumuona kwa mwanaume mwingine.

Kwa mujibu wa mashuhuda, kijana huyo aliyefahamika kwa jina la Edwin K., alionekana majira ya saa nne asubuhi akitembea bila shati katika mitaa ya Mbezi huku mwili wake mzima ukiwa umeandikwa jina “Sheila” kwa wino mkubwa wa kudumu.

Maneno hayo yaliandikwa kwenye kifua, mgongo, mikono hadi mapajani. Alionekana pia ameshika ua la waridi mkononi, akisema linamwakilisha upendo wa milele ambao hauwezi kufutika.

“Tulifikiri ni maigizo ya mitandaoni,” alisema mlinzi wa duka jirani. “Lakini alipoanza kulia hadharani na kueleza alivyomuoa moyoni, tukajua hapa kuna jambo kubwa.”

Kwa mujibu wa majirani wa karibu, Edwin alikuwa kwenye uhusiano wa miaka mitatu na Sheila kabla ya kuachana miezi minne iliyopita baada ya binti huyo kudai kutopata msukumo wa kimapenzi kutoka kwake. Tangu kuachwa, Edwin amekuwa akijitenga kijamii, akiacha kazi na kukataa kuzungumza na mtu yeyote isipokuwa picha za binti huyo alizobandika chumbani kwake. Soma zaidi hapa 

Related Posts