Nature
Jesca John Magufuli kuwa Mbunge wa Viti Maalum

Jesca Magufuli Achaguliwa Mbunge wa Viti Maalum Kupitia UVCCM

Wajumbe wa Mkutano Mkuu Maalum wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa 2025 wamemchagua Jesca John Magufuli kuwa Mbunge wa Viti Maalum kupitia kundi la Vijana kutoka Tanzania Bara.

Katika matokeo yaliyotangazwa alfajiri ya leo, Agosti 2, 2025, Jesca ameshika nafasi ya pili kwa kupata kura 391 kati ya kura 24,666 zilizopigwa na wajumbe kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania Bara. Mchakato huo wa uchaguzi umeelezwa kuwa wa wazi na wa haki, huku ukihusisha ushindani mkali kutoka kwa wagombea kadhaa wenye ushawishi mkubwa kisiasa.

Uchaguzi huo umefanyika kuanzia Agosti 1 hadi 2, 2025 katika Ukumbi wa Jiji, Mtumba – Dodoma, ambapo wagombea walichuana vikali kuwania nafasi hizo muhimu kwa ajili ya kuwakilisha kundi la vijana bungeni kupitia tiketi ya CCM. Tukio hilo pia limehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa chama, wazee wa chama, pamoja na wawakilishi wa taasisi za vijana.

Jesca ni miongoni mwa vijana waliopata ushindi mkubwa wa kisiasa mwaka huu, na jina lake limeendelea kuvuma katika mijadala ya kisiasa nchini kutokana na kuwa mtoto wa aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano, Hayati Dkt. John Pombe Magufuli. Pamoja na nasaba hiyo, wengi wanamsifu kwa nidhamu, ufuatiliaji wa masuala ya kijamii na uwezo wake wa kujieleza vyema mbele ya hadhira.


Ushindi wake unatazamwa na wengi kama ishara ya kizazi kipya ndani ya CCM kinachojitokeza kuchukua nafasi za juu za uongozi kupitia jukwaa la UVCCM. Wanachama wengi wameeleza matumaini kuwa Jesca atakuwa sauti ya vijana bungeni na chachu ya mabadiliko chanya kwa taifa.

Related Posts