Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limeingilia na kusitisha mkutano wa waandishi wa habari uliokuwa umeandaliwa na Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Bara, John Heche, katika Hoteli ya Seashells Millennium Tower, jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kaimu Mkuu wa Upelelezi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) George Bagyemu, polisi walifika kwenye ukumbi wa hoteli hiyo mnamo saa chache kabla ya mkutano kuanza rasmi na kuamuru waandishi wa habari waliokuwepo kutawanyika mara moja.

Aidha, waliamuru Brenda Rupia, ambaye alikuwa msimamizi wa mkutano huo, kuondoka ukumbini papo hapo.

ACP Bagyemu alieleza kuwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimezuiwa kwa sasa kufanya shughuli zozote za kisiasa kufuatia agizo la Mahakama Kuu ya Tanzania.

Mahakama hiyo, kupitia Masjala Ndogo ya Dar es Salaam, ilitoa agizo hilo Juni 10, 2025, ikiwa ni hatua ya muda wakati kesi ya msingi dhidi ya chama hicho ikisubiri kuanza kusikilizwa rasmi tarehe 24 Juni 2025.

Licha ya maelezo hayo, Brenda Rupia aliwaeleza askari kuwa mkutano huo haukuwa wa chama bali ni wa mtu binafsi Makamu Mwenyekiti John Heche ambaye alitaka kuzungumza na wanahabari kuhusu masuala mbalimbali ya kitaifa.

Hata hivyo, polisi walisisitiza kuwa, kwa kuwa Heche ni kiongozi wa CHADEMA na kutokana na zuio lililopo mahakamani, hata shughuli za mtu binafsi zinazoonekana kuwa na mwelekeo wa kisiasa haziruhusiwi kwa sasa.

Tukio hili limeibua maswali kuhusu uhuru wa vyombo vya habari na nafasi ya wanasiasa kutoa maoni yao katika mazingira ya kidemokrasia, hasa ikizingatiwa kuwa mkutano huo ulikuwa na sura ya mawasiliano na umma kupitia vyombo vya habari, si mkutano wa hadhara wa kisiasa.

Hadi sasa, Jambo TV inafanya jitihada za kumtafuta Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, kwa maelezo zaidi juu ya msingi wa zuio hilo na iwapo hatua hiyo ni sehemu ya utekelezaji wa agizo la mahakama au ni tafsiri ya ndani ya mamlaka ya usalama.

Wachambuzi wa masuala ya siasa na sheria wanasema tukio hili linaweza kuwa kielelezo cha changamoto kubwa zinazolikabili taifa katika kuhakikisha usawa wa kisiasa na uhuru wa kujieleza, hasa katika kipindi ambacho vyama vya upinzani vinaendelea kukabiliana na vizingiti vya kisheria na kiutendaji.


Alikataa kuolewa ili amkomboe mama yake... Lakini mama ndiye aliyemuuza!

GORYANAH –Hii ni story ya Moto Sana yenye hisia na Mafunzo, binti jasiri anayepambana na siri nzito, umaskini na hatari kubwa kwa ndoto zake! Pakua app yetu ufurahie Sehemu ya 1 Hadi ya 5,na mwendelezo wake kila JUMAMOSI SAA MOJA KAMILI JIONI BURE!

BONYEZA HAPA KU DOWNLOAD.

Ukiona ujumbe wa allow notification bonyeza allow ili uwe mwanafamilia.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *