John Heche: Serikali Imuachie Tundu Lissu Bila Masharti
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kwa mara nyingine tena kimetoa wito kwa Serikali kumuachia kutoka gerezani Mwenyekiti wa Chama hicho, Tundu Lissu, bila masharti yoyote ili arudi uraiani kuendeleza kampeni ya ukombozi na mabadiliko.
Akiongea leo June 30,2025, Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, Bara, John Heche amesema ““Tumekataa na haiwezekani Serikali na vyombo vyote kupuuzia mahitaji ya Watanzania ya kuwa na mabadiliko kwenye mifumo ya uchaguzi, katika hatua hii tunawasihi Watanzania muoneshe hisia zenu ili Serikali na vyombo vyote vijue kuwa mmekasirika na hamjapendezwa na dharau hii, endeleeni kupambana kudai haki hii kila mmoja na kamwe tusikate tamaa”
ALSO READ | Tazama Live Kesi ya Tundu Lissu Leo Mahakama ya Kisutu
“Haiwezekani nchi ikiwa katika joto la
mahitaji ya maboresho ya mifumo ya uchaguzi, Rais kwenye hotuba yake ya June 27,2025 anapuuzia kabisa kuzungumzia jambo hili, sasa msifiche hisia zenu na ijulikane kuwa no reforms no election ni vuguvugu la kweli”
Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo Bonyeza Hapa

