Mgombea wa ubunge katika jimbo la Arusha Mjini anayejulikana kwa majina ya Mrisho Gambo ametoa taarifa nzito kwa wananchi wa jimbo hilo ikiwa ni muda mfupi mara baada ya kuchukua ya fomu ya kutaka kugombea nafasi hiyo kuelekea kwenye uchaguzi mkuu ambao utafanyika mwezi Octoba mwaka huu.

Mrisho Gambo ndiye mbuge aliyetoka madarakani na sasa amefanya maamuzi magumu ya kugombea tena ambapo sasa atakutana na upinzani kutoka kwa aliyekua mkuu wa mkoa wa Arusha anayejulikana kwa majina ya Paul Makonda.

Mrisho Gambo mara baada ya kukamilisha mchakato wa kuchukua fomu ya kugombea siku ya jana Jumapili tarehe 29 Juni, alieleza mambo machache ambayo yamemsukuma kugombea tena nafasi ya ubunge katika jimbo la Arusha mjini kwa awamu ya pili mfululizo.

Gambo katika taarifa yake alieleza wazi kwamba amefanya maamuzi magumu ya kugombea ubunge kwa awamu hii kwa sababu kwanza hana mashaka na elimu yake na ana vyeti vyote ambavyo vinaonyesha uhalisia kwamba yeye ni msomi aliyekamilika.

Taarifa hii kutoka kwa Gambo bila shaka itakua imelenga kumsema vibaya Paul Makonda ambaye miaka kadhaa iliyopita aliwai kuingia kwenye utata Kuhusu elimu na jina lake halisi

Gambo ameamua kuibua hoja hiyo upya akiwa anaamini kwamba hii inaweza kuwa silaha ya kumchapia Makonda akiwa kama mpinzani wake mkubwa kuelekea kwenye kura za maoni za ndani ya Chama Cha Mapinduzi yaani CCM.

Gambo pia amedokeza kwamba mpango wake wa kugombea umebeba dhana ya kutaka kuendelea kufanya maendeleo katika jimbo hilo ikiwa ni pamoja na kuendeleza miradi anbayo haijakamilika kwa muda wa miaka mitano ambayo alikuwa madarakani.


Alikataa kuolewa ili amkomboe mama yake... Lakini mama ndiye aliyemuuza!

GORYANAH –Hii ni story ya Moto Sana yenye hisia na Mafunzo, binti jasiri anayepambana na siri nzito, umaskini na hatari kubwa kwa ndoto zake! Pakua app yetu ufurahie Sehemu ya 1 Hadi ya 5,na mwendelezo wake kila JUMAMOSI SAA MOJA KAMILI JIONI BURE!

BONYEZA HAPA KU DOWNLOAD.

Ukiona ujumbe wa allow notification bonyeza allow ili uwe mwanafamilia.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *