Klabu ya Al-Ittihad Yailipa Wydad Bilioni 3.9 Mauzo ya Mchezaji Aziz K

Klabu ya Al-Ittihad Yailipa Wydad Bilioni 3.9 Mauzo ya Mchezaji Aziz K
Klabu ya Al-Ittihad Yailipa Wydad Bilioni 3.9 Mauzo ya Mchezaji Aziz K

Miamba ya soka nchini Libya, Al-Ittihad Club, imekamilisha rasmi malipo ya ada za uhamisho kwa klabu ya Wydad Athletic Club ya Morocco kwa ajili ya nyota wao wapya wawili.

Malipo hayo ya jumla ya Dola milioni 1.4 (Sh3.9 bilioni) yamehusisha:

Stephane Aziz Ki: Ada ya $800,000 (Sh2.04 bilioni).

Thembinkosi Lorch: Ada ya $600,000 (Sh1.53 bilioni).

Kukamilika kwa miamala hiyo kunahitimisha mchakato wa usajili wa wachezaji hao ambao tayari wameanza kuitumikia klabu hiyo ya Tripoli katika msimu wa 2025/26.

Aziz Ki, kiungo wa zamani wa Yanga, amekabidhiwa jezi namba 22 (huku vyanzo vingine vikitaja namba 32), wakati Thembinkosi Lorch akivaa jezi namba 11.

Related Posts