Nature

Kocha Ibenge ‘Mpanzu Ndio Mchezaji Hatari Ligi Kuu Tanzania’

Kocha wa Azam FC, Florent Ibenge, amemwaga sifa kwa winga wa Simba SC, Elie Mpanzu, akimtaja kama miongoni mwa wachezaji hatari zaidi katika Ligi Kuu Tanzania.

Ibenge amesema anamfahamu Mpanzu kwa muda mrefu tangu akiwa DR Congo, akieleza kuwa ubora wa mchezaji huyo unamfanya kuwa tishio kwa timu yoyote, hasa pale anapokuwa katika kiwango chake cha juu.

Amefafanua kuwa Mpanzu ana kasi, nguvu, ubunifu na uwezo wa kubadilisha mwelekeo wa mchezo muda wowote, jambo linalomlazimu kocha yeyote kumzingatia katika maandalizi ya mechi.

Kocha Ibenge ametoa kauli hizo leo wakati akiingia kwenye maandalizi ya kukabiliana na Simba yenye Mpanzu, akisisitiza kuwa licha ya kumheshimu mchezaji huyo, ameandaa kikosi chake ipasavyo kupambana na changamoto hiyo.

Mechi hiyo inatarajiwa kuwa yenye ushindani mkubwa kutokana na uimara wa vikosi vyote na umuhimu wa pointi katika mbio za Ligi Kuu msimu huu

Related Posts