Tunacheza fainali nyingine ya pili mfululizo kwenye mashindano haya, tuna uzoefu wa kutosha na mechi za fainali na tumejiandaa vizuri kwa ajili ya mchezo huo.
Sina uzoefu wa kutosha wa kucheza dhidi ya Simba kwa sababu sikuwahi kukutana nao kabla lakini nimewahi kukutana na Yanga mwaka 2017.
Tuna wachezaji wawili ambao wamerejea kikosini baada ya kutoka kwenye majeraha lakini tutajua kama watakuwa kwenye kikosi au vinginevyo.
– Mouin Chaaban, Kocha RS Berkane