Kocha wa klabu ya Yanga Pedro Goncalves Ajikosesha Ushindi Mwenyewe

Kocha wa klabu ya Yanga Pedro Goncalves leo ameikosesha alama tatu Yanga sc kutokana na kushindwa kucope na mahitaji ya mchezo kulingana na wakati

Pedro alianza na Boka ili anufaike nae kwenye kushindana nguvu na kasi dhidi ya mawinga wa Ahly kitu kilichofanya atumie nguvu kubwa sana na kuonyeshwa kadi ya njano kipindi cha kwanza

Kipindi cha pili hakua na matumizi makubwa ya nguvu kwakua tayari alikua na yellow card pia kasi yake ilipungua kwa sababu first alitumia nguvu kubwa kushindana na mawinga wa Ahly

Nilitegemea mapema kipindi cha pili umuingize Mohamed Hussein pia timu izuie kwenye midblock na sio kwenye low block jambo lililokua linafanya Ahly wacheze karibu na eneo la hatari la Yanga hivyo kutengeneza nafasi nyingi na Yanga walikua mbali na lango hivyo kua ngumu kufanya Counter attack

Makosa mawili ya kuchelewa kumtoa Boka na kuirudisha timu nyuma yamefanya Yanga kudodosha alama 2

Related Posts