Nature

KOCHA wa zamani wa Yanga, Sead Ramovic Aipiga Mkwala Singida Black Stars

KOCHA wa zamani wa Yanga, Sead Ramovic ambaye kwa sasa anainoa CR Belouizdad ya Algeria ameichimba mkwara Singida Black Stars ikiwa ni siku chache kabla mechi ya kwanza ya hatua ya makundi kati ya timu hizo katika Kombe la Shirikisho Afrika.

Sead Ramovic 🗣.”Najua Singida ni timu mpya kwenye michuano hii, lakini hawatakuja hapa kutembea. Wanakuja kupambana na nami pia nataka hilo. Uzoefu wangu Tanzania najua utasaidia. Najua aina yao ya uchezaji ilivyo, nimeiona ni moja ya timu shindani.”

“Tunawaheshimu, lakini hatutawaacha wapumue. Hapa ni nyumbani kwetu na tutajua namna ya kuwakaribisha.”

Related Posts