“Tanzania na Morocco kuna utofauti mkubwa…Binafsi sehemu ya maisha yangu pia yapo hapa Morocco, namfahamu Walid (Regragui), nakumbuka wakati niko FUS Rabat alikuwa ananisumbua kimbinu, ni kocha mzuri tumesumbuana sana wakati wa ukuaji wetu kama makocha.” – Kocha wa Tanzania Miguel Gamondi akimzungumzia Kocha wa Morocco Walid Regragui.
Tanzania itakutana na Morocco kesho kwenye mchezo wa hatua ya 16 bora AFCON2025 kwenye dimba la Prince Moulay Abdellah kuanzia saa 1:00 usiku
