
Lamine Yamal Mchezaji Bora wa Msimu wa Ligi Kuu Uhispania (La Liga)
Winga wa Kimataifa wa Uhispania na klabu ya Barcelona, Lamine Yamal ametajwa rasmi kuwa Mchezaji Bora wa Msimu wa Ligi Kuu Uhispania (La Liga) baada ya kusaidia klabu hiyo kutwaa ubingwa wa Ligi hiyo msimu wa 2025/2026.
Yamal 19, ametwaa tuzo hiyo inayotolewa na Laliga kwa ushirikiano na kampuni ya michezo ya video ya EA Sports baada ya kuifungia Barcelona magoli 16 na kutoa pasi za mwisho (assists) 11 kwenye michezo 28 aliyocheza kwenye ligi hiyo.
ALSO READ | Hivi ndivyo Dk Nchimbi anavyoweza kurudi CCM
