Licha ya Kuwafunga Stade Malie SIMBA Yamaliza Safari ya Ligi ya Mabingwa Ikiwa ya Mwisho

Wekundu wa Msimbazi, Simba Sc wamepata ushindi wa kwanza kwenye hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika (CAFCL) kufuatia ushindi wa 1-0 dhidi ya vinara wa kundi D, Stade Malien katika dimba la Benjamin Mkapa.

Kwenye mchezo mwingine wa kundi hilo, Esperance de Tunis imeilaza Petro De Luanda mabao 2-0 na kuungana na Stade Malien kwenye hatua ya robo fainali huku Simba Sc na Petro Luanda kuaga mashindano hayo.

FT: Simba Sc 🇹🇿 1-0 🇲🇱 Stade Malien
⚽ 04’ Anicet Oura

Esperance Tunis 🇹🇳 2-0 🇦🇴 Petro De Luanda
⚽ 46’ Diakite
⚽ 82’ Diarra

MSIMAMO KUNDI D

🇹🇿 Simba Sc – pointi 5 (-2).

🇲🇱 Stade Malien – pointi 11 (+3)

🇹🇳 Esperance – pointi 9 (+2)

🇦🇴 Petro Luanda – pointi 6 (-3)

Related Posts