Lissu atajwa tatu bora kuwania tuzo ya haki za binadamu EU

Lissu atajwa tatu bora kuwania tuzo ya haki za binadamu EU
Lissu atajwa tatu bora kuwania tuzo ya haki za binadamu EU

Lissu atajwa tatu bora kuwania tuzo ya haki za binadamu 2026
Bunge la Ulaya limemtaja mwanasiasa wa Tanzania, Tundu Lissu, kuwa miongoni mwa wagombea watatu wa mwisho wa Tuzo ya Sakharov ya Uhuru wa Mawazo kwa mwaka 2026, inayotambua mchango wa kipekee katika kutetea haki za binadamu, demokrasia na uhuru wa msingi.

Lissu anaingia katika hatua ya mwisho ya tuzo hiyo pamoja na Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) na maofisa wake, pamoja na Taraneh Rahimi na Romina Rahimi kutoka Iran.

Tuzo ya Sakharov hutolewa kila mwaka na Bunge la Ulaya kwa watu binafsi au mashirika yanayoonyesha ujasiri wa kipekee katika kutetea haki za binadamu na uhuru wa msingi duniani.

Kwa mwaka 2026, kamati za Bunge la Ulaya zinazoshughulikia Mambo ya Nje na Maendeleo zilipangiwa kupigia kura wagombea hao watatu Oktoba 19, mjini Strasbourg, Ufaransa.

Baada ya hatua hiyo, Mkutano wa Marais wa Bunge la Ulaya umepangiwa kuamua mshindi wa tuzo hiyo Oktoba 22, 2026.

Mwaka 2025, tuzo hiyo ilitolewa kwa Andrzej Poczobut, mwandishi wa habari na mwanaharakati wa jamii ya Wapolandi nchini Belarus, pamoja na Mzia Amaglobeli, mwandishi wa habari kutoka Georgia ambaye alitambuliwa kama mfungwa wa kisiasa wa kwanza mwanamke nchini humo tangu taifa hilo lipate uhuru.

Uteuzi wa Lissu katika orodha ya mwisho unaweka jina la Tanzania miongoni mwa wagombea wanaotambuliwa na Bunge la Ulaya kwa mchango wao katika masuala ya haki za binadamu na uhuru wa msingi.

Related Posts