Anaandika @kelvinrabson_
Nafikiri mikakati ya kocha wa SBS “David Ouma” ilikuwa sahihi kabisa ya jinsi gani ya kukabiliana na Simba .
A) Hakikisha unazuia vizuri kwa kulinda muundo wako wa ulinzi usiharibike ( mstari wao wa ulinzi ulikuwa juu dhumuni kuwafanya Simba mda mwingi kucheza wakiwa kwenye nusu yao )
B) Waliweka mtego wa kushambulia kwa “Counter Attacks” mawinga wao wanaombea mpira wakiwa ndani “Half Spaces” + Koffi & Imoro wanashambulia nafasi nyuma ya FBs wa Simba , kwa nyakati nyingi walifanikiwa lakini maamuzi ya pasi zao za mwisho ndio yaliwaangusha .
✍️ Kama dakika 30 za kipindi cha kwanza SBS walifanikiwa kwenye plan yao ( Kuzuia na idadi kubwa ya wachezaji , kuwa na muundo mzuri wa uzuiaji pia weka presha vizuri kwenye mpira ) …. Baada ya hapo Simba walionesha action gani ?
1: Badilisha upande kwa haraka kwenye nafasi na maeneo sahihi : mpira ulikuwa unatembea kwa haraka kutoka sehemu moja kwenda nyingine , dhumuni ni kupata nafasi kwenye mpira na maeneo hatarishi .
2: Rotations & Movements : kama kawaida yao wachezaji wote wa mbele + FBs wanafanya rotation kwenye nafasi zao bila kuharibu muundo wao wa uchezaji na walifanya movements za hatari nyuma ya walinzi wa SBS …. Kwanini ilikuwa hivo ?
✍️ Kwasababu SBS mstari wao wa ulinzi ulikuwa juu ( Hawakuzuia wakiwa chini sana ) .
✍️ Nafikiri “Fadlu Davids” Kipindi cha pili aliamua kuifunga game : Simba bila mpira hawakuweka presha kuanzia juu bali walirudi chini haraka kuzuia kwenye ( Midblock ) wakiwa na 5-4-1 kuwafanya SBS kukosa nafasi wakivuka kwenye mstari wa kati na walifanikiwa .
NOTE :
1: Yule Koffi “Fullback” wa SBS kacheza game bora sana : Energy yake ✅
2: Morice Chukwu , Bada + CBs wa SBS 🔥 wote walikuwa na game nzuri sana .
3: Steven Mukwala goli lake la 12 kwenye NBCPL ✅
4: Nashon ana bahati sana , bila kadi nyekundu
5: SIMPLE SBS walistahili Penalti 2 kwenye mchezo huu .
6: Sowah aliwapa wakati mgumu sana Malone na Chamoue
7: Simba unawaona kabisa mechi Vs Berkane imekomba energy yao .
FT : Simba 1-0 SBS