Nature

Marekani Yuko na Israel, Nani Anaisaidia Iran?


Israel inaishambulia Iran na karibu imetamka wazi wazi lengo halisi la operesheni hiyo: mabadiliko ya utawala katika Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Marekani yenyewe rasmi sasa imeamua kuisaidia Israel, mshirikia wake wa muda mrefu.

Mwishoni mwa wiki Marekani ilifanya mashambulizi kwenye maeneo matatu ya nyuklia nchini Iran, ambayo ni Fordo, Natanz na Esfaha

Kinachoendelea kwa Hezbollah nchini Lebanon, kuanguka kwa Bashar al-Assad nchini Syria, na vita na Hamas, kumeitingisha Iran. Hata kabla ya vita ya sasa dhidi ya Israel , Iran haikuonekana kuwa na washirika wengi, iwe katika kanda au duniani.

Sasa iko kwenye vita kamili dhidi ya mataifa makubwa na yenye nguvu kijeshi, Israel na mshirika wake Marekani, Je nani anamuunga mkono Iran? anapigana vita kipweke?

Urusi

Urusi, mmoja wa washirika wakuu wa Iran, ilikuwa miongoni mwa nchi za kwanza kulaani mashambulizi ya Israel na kutoa wito wa kupunguza mara moja hali ya mvutano na kusitisha mapigano. Uturuki na China, ambazo pia zina uhusiano na Iran, zilichukua msimamo kama huo. Lakini misimamo hii mikali haikusababisha hatua yoyote ya kivitendo.
Hanna Note, Mkurugenzi wa mpango wa Eurasia katika Kituo cha utafiti wa kutokukua kwa silaha za nyuklia, aliiambia BBC: “Urusi haijatoa msaada wowote wa kijeshi kwa Iran. Bila shaka, hakuna aliyetarajia. Urusi na Iran zilisaini makubaliano ya ushirikiano kamili mnamo Januari, lakini ilikuwa wazi tangu mwanzo kwamba makubaliano hayo hayakujumuisha msaada wa kijeshi iwapo kutatokea vita.

Mwaka jana, wakati Israel ilipoishambulia Iran kwa mara ya kwanza, Teheran ilitarajia Moscow ingeipelekea mifumo ya kisasa zaidi ya ulinzi wa anga, lakini hilo halikutokea.

Urusi ingeweza kweli kuipatia Iran vifaa vya ulinzi wa anga, kama vile mfumo wa masafa mafupi wa Pantsir-S1, kulinda mifumo ya ulinzi ya masafa marefu au mitambo mingine dhidi ya makombora ya Israel. Urusi pia ingeweza kuuza idadi ya ndege za kivita za Su-35, ambazo hapo awali zilitengenezwa kwa ajili ya kuuzwa Misri na mkataba wake ulikatishwa, kwenda Iran, ambayo ilikuwa imeeleza nia ya kuzinunua.

“Lakini haikutokea,” anasema Note. “Labda kwa sababu Urusi haikuweza au haikutaka. Au labda sababu zote mbili zilikuwa kweli kwa wakati mmoja.” Wataalamu wanaamini kwamba kama Urusi ingetaka kutoa silaha hizo kwa Iran sasa, ingelikuwa imechelewa mno, kwa sababu Israel imetangaza rasmi kudhibiti anga ya Iran.

Putin alisema katika mkutano na watendaji wa mashirika ya habari za kigeni mnamo Juni 18 kwamba Iran haikuomba hata msaada kutoka Urusi katika siku za hivi karibuni. Kuhusu mifumo ya ulinzi wa anga, alisema kuwa Urusi ilikuwa imetoa ushirikiano kwa “marafiki wa Iran,” lakini akaongeza kwamba “washirika wetu hawakuonyesha nia kubwa.”

Wataalamu wanasema mikono ya Urusi imefungwa na vita nchini Ukraine, ambayo inabaki kuwa kipaumbele kwa Putin. Fabrice Balanche wa Taasisi ya Washington kwa Sera ya Mashariki “Hatujui hasa Putin na Trump walisema nini kuhusu Ukraine,” anasema.

Hanna Note anasema kuwa maafisa wa Urusi wanaelewa wazi kuwa Israel ina nguvu zaidi katika vita hivi na hawataki kuweka nguvu kwa upande ambao unaonekana kuzidiwa ama utapoteza.

Margarita Simonyan, mmoja wa watu wenye ushawishi Urusi, aliandika kwenye mtandao wa kijamii wa X siku chache zilizopita: “Mwenye nguvu zaidi ndiye mwenye haki.” “Hii ndiyo hali halisi nchini Urusi,” anasema. “Putin anavutiwa zaidi na watu wanaoshinda kuliko wanaoshindwa.”

China
Kujibu shambulio la Israel, msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China, Lin Jian alisema nchi yake “ina wasiwasi mkubwa kuhusu mashambulizi ya Israel dhidi ya Iran na ina wasiwasi mkubwa kuhusu matokeo mabaya yanayoweza kutokea kutokana na vitendo hivi.” Lin aliongeza kuwa Beijing inapinga “uvunjifu wowote wa mamlaka, usalama, na uadilifu wa eneo la Iran” na “vitendo vinavyochochochea mvutano na kuongeza mzozo.”

China inabaki kuwa mnunuzi mkubwa zaidi wa mafuta ya Iran, ambayo iko chini ya vikwazo vya Marekani. Vikwazo vinaweka mipaka ya biashara kati ya nchi hizo mbili, ndiyo maana Iran inapokea uwekezaji mdogo wa Kichina kuliko nchi za Ghuba. Lakini hili halijaizuia Iran kuendelea na juhudi zake za kuimarisha uhusiano wake na Beijing. Mnamo 2023, Teheran ilijiunga na Shirika la Ushirikiano la Shanghai, ikitafuta kuimarisha uhusiano wa kiuchumi kati ya nchi hizo mbili.

Lakini Beijing ni taifa lenye maslahi ya kimataifa yanayozuia migogoro ya kigeni kuathiri maslahi yake. “China inazingatia sana kuweka sawa uhusiano wake kwa kutojiweka sana karibu na Iran kiasi kwamba inaweza kuharibu uhusiano wake na wapinzani wa Teheran. China haijataka kucheza jukumu kubwa katika siasa na usalama wa Mashariki ya Kati kwa sababu inataka kuzingatia upande wa biashara na kuepuka kuathiriwa na migogoro hii,” Thomas Juneau, profesa katika Shule ya Uzamili ya Masuala ya Umma na Kimataifa ya Chuo Kikuu cha Ottawa, aliiambia BBC Mundo Oktoba.

Mansour Farhang, profesa mstaafu wa sayansi ya siasa katika Chuo cha Bennington huko Vermont, alikubali: “China ina uhusiano mzuri sana wa kibiashara na kila nchi katika kanda. Sera yake ya mambo ya nje huko Mashariki ya Kati inafanana na ya mfanyabiashara.”

Korea Kaskazini na ushirikiano wenye mipaka
Pyongyang na Teheran zina historia ya biashara ya silaha kwa mafuta tangu miaka ya 1980 wakati wa Vita ya Iran na Iraq. Korea Kaskazini ilituma silaha na makombora, wakati Iran ilituma mafuta na mbolea.

Kwa kweli, wataalamu wanaamini kwamba kombora la masafa ya kati la Shahab-3 la Iran ni toleo ambalo Teheran ilitengeneza kutoka kombora la No Dong 1 la Korea Kaskazini, ambalo ililipata katika miaka ya 1990.

Uhusiano kati ya nchi hizo mbili umedumishwa hadi sasa, lakini una mipaka yake kutokana na vikwazo vikali ambavyo nchi zote mbili ziko chini yake. Kulingana na wachambuzi, umuhimu wa kisiasa na hadhi yao kama “nchi zilizotengwa” zimewaongoza kudumisha kiwango cha juu zaidi cha ushirikiano.

Ingawa zimeidumisha uhusiano rasmi tangu mwaka 1960, kutokana na hadhi yao kama waanzilishi wa OPEC, hakukua na ukaribu sana hadi pale serikali za Hugo Chávez na Mahmoud Ahmadinejad ndipo uhusiano kati ya Iran na Venezuela ulikua kwa kasi kubwa. Katika miaka ya 2000, Caracas na Teheran zilianzisha muungano wa kimkakati na kusaini zaidi ya makubaliano 180 ya pande mbili katika maeneo mengi, yenye thamani ya zaidi ya dola bilioni 17 za Marekani.

Mengi ya makubaliano hayo yalibaki kwenye karatasi, huku mengine yakitekelezwa nusu tu na kisha kuachwa. Baada ya kifo cha Chávez mwaka 2013, uhusiano ulidhoofika, lakini uliimarika tena wakati Marekani ilipoweka vikwazo vya mafuta kwa Venezuela miaka mitano baadaye.

Iran imeisaidia Venezuela kwa kutoa viambato vya kemikali vinavyohitajika kuzalisha petroli kwa kubadilishana na dhahabu ya Venezuela. Nchi zote mbili pia zilikuwa zikibadilishana mafuta mazito ya Venezuela kwa mafuta mepesi ya Iran ambayo yanaweza kutumika kusaidia uzalishaji wa mafuta nchini Venezuela.

Kufuatia mashambulizi ya Israel dhidi ya Iran, Rais wa Venezuela Nicolás Maduro alithibitisha tena kuunga mkono na mshikamano wake na Iran. “Tunathibitisha kwa dhati mshikamano wetu kamili na watu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, watu wa Palestina, watu wa Syria, watu wa Lebanon, watu wa Yemen, na watu wote wa jamii ya Kiislamu na Waarabu,” rais huyo alisema katika hafla iliyoonyeshwa katika televisheni. Zaidi ya matamshi, wataalamu wanaamini msaada wa Venezuela kwa Iran ni ishara na hauna faida kubwa kwa taifa hilo la Kiislamu.

Cuba, Nicaragua, Bolivia
Huko Amerika Kusini, Iran ilikuwa na uhusiano wa muda mrefu na Cuba, ulioundwa ndani ya mfumo wa harakati za nchi zisizofungamana na upande wowote, lakini uhusiano wa karibu umeendelea katika miaka ya hivi karibuni, hasa kutokana na kuanzishwa kwa muungano wa karibu na Venezuela na washirika wake wa ALBA, ambao unajumuisha Cuba yenyewe, pamoja na Nicaragua na Bolivia.

Nchi hizi zinashirikiana na Teheran chuki kali dhidi ya Marekani na huwa zinaungana kidiplomasia, zikiratibu misimamo yao ndani ya mashirika mbalimbali ya kimataifa.

Kulingana na Juneau, kama ilivyo kwa Venezuela, msaada wa nchi hizi kwa Iran pia ni ishara. “Viongozi wa Iran na viongozi wengine wa nchi hizi wanapenda kukutana na kufanya mikutano na waandishi wa habari wakikosana Marekani na kudai kuwa washirika katika kupinga ukoloni, ubeberu, n.k., lakini kwa vitendo, kutoka kwa mtazamo wa kijeshi na usalama, wanaweza kuisaidia Iran katika mapambano yake ya sasa dhidi ya Israel na Marekani? Nadhani jibu ni, kwa kiasi kikubwa, hapana.”

Upweke wa Kimkakati?
Katika makala ya kitaaluma iliyochapishwa mwaka 2014, Juneau alielezea “upweke huu wa kimkakati.” “Iran iko peke yake duniani. Kutengwa kwake kwa kimkakati kunatokana na mambo ya kimuundo yanayohusiana na nafasi yake katika mifumo ya kikanda na kimataifa na kwa kiasi kikubwa hakuathiriwi na matendo ya yeyote anayeiongoza nchi hiyo,” aliandika.

“Msimamo wake wa kimataifa haufanyi ushirikiano na mataifa mengine usiwezekane, wala haubashiri hali ya migogoro ya kudumu na majirani zake. Upweke wa kimkakati, hata hivyo, unaeleza ni kwa nini Iran ina maslahi machache sana ya kawaida na majirani zake na kwa nini ushirikiano ni mgumu na unahitaji gharama kubwa kufikiwa,” aliongeza.

Sababu kadhaa zinachangia kutengwa kwa Iran, ikiwemo ukweli kwamba ndiyo nchi pekee ya Kiajemi duniani. Kwa kuongezea, ingawa kuna takriban nchi 50 zenye Waislamu walio wengi, ni chache tu kati yao zenye jamii ya Shia, dhehebu la Kiislamu ambalo Iran inalifuata, likiwa linawakilisha idadi kubwa ya watu.

Nchi hii pia inaathiriwa na eneo lake la kijiografia, kwani iko katika eneo la majirani wenye nguvu na malengo makubwa ambayo yamesababisha vita na ushindani mkubwa hapo zamani.

Na vita vya hivi karibuni kati ya Israel na washirika wa Iran, Hamas na Hezbollah, vilivyozuka baada ya kundi la Kipalestina kushambulia eneo la Israel mnamo Oktoba 7, 2023, na kuua takriban watu 1,200 na kuwateka nyara wengine 251, vimeiacha Jamhuri ya Kiislamu ikiwa imetengwa na isiyolindwa zaidi kuliko hapo awali.

Related Posts

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *