Mary wa Mwijaku Ahukumiwa, Atupwa Jela Baada ya Kushindwa Kulipa Fine

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imewahukumu wanafunzi watatu wa vyuo vikuu tofauti kulipa faini ya Shilingi milioni 15 kila mmoja, au kutumikia kifungo jela, baada ya kupatikana na hatia kwa makosa saba, yakiwemo kumpiga na kumjeruhi mwenzao, kutoa vitisho vya kuua, pamoja na kusambaza taarifa za uongo.

Hukumu hiyo imetolewa leo, Disemba 22, 2025, na Hakimu Mkazi Mkuu Gwantwa Mwankuga.

Wanafunzi waliopatikana na hatia ni Mary Matogolo (Chuo Kikuu cha Dar es Salaam – UDSM), Ryner Mkwawili (Chuo Kikuu Ardhi), na Asha Juma (Chuo cha Uhasibu – TIA).

Mpaka kufikia saa 10:48 alasiri, Ryner na Asha walikuwa wamelipa faini na kuachiwa huru, huku Mary Matogolo akikabidhiwa kwa maafisa magereza baada ya kushindwa kulipa faini hiyo.

Related Posts