Haya hapa ni maswali matano ambayo ukisikia mwanamke anakuliza mara kwa mara, ujue kuna kitu kinachemka moyoni mwake:
- “Upo Single au Una Mtu?”
Hili linaweza kuonekana kama swali la kawaida, lakini mwanamke anayevutiwa na wewe hataki kujiingiza kwenye maumivu bure. Anapotaka kujua hali yako ya mahusiano, mara nyingi ni kwa sababu anapima nafasi yake kwako. - “Unapenda Mwanamke wa Aina Gani?”
Hili ni swali la kuchungulia vigezo vyako. Mwanamke akikuuliza hivi, anataka kujilinganisha na hayo maelezo, ili aone kama ana nafasi ya kuingia kwenye maisha yako kimahaba.
- “Mbona Hujawahi Kuwa na Girlfriend? Au Wewe ni Mtoto wa Mama Sana?”
Swali hili linakuja kwa njia ya utani, lakini lina lengo la kupima hisia zako na kama uko tayari kuingia kwenye mahusiano. Wakati mwingine ni njia ya kuchokoza mazungumzo ya kimapenzi. - “Ulikuwa Wapi Jana Usiku?”
Usiichukulie kawaida hii. Hili ni dalili ya wivu wa chini kwa chini. Mwanamke akianza kufuatilia ratiba zako, anamaanisha anajali – na mara nyingi anaanza kujiwekea picha kuwa wewe ni mtu wake. - “Ungependa Tuende Wapi Weekend?”
Swali kama hili linaonyesha anataka kukaa karibu na wewe kwa muda zaidi, mahali pa faragha au pa kufurahia maisha. Mwanamke anayepanga muda na wewe kwa hiari yake, hana shaka kuwa anajisikia vizuri akiwa karibu na wewe.

