Mwanaume wa Miaka 50 Afariki Akifanya Mapenzi na Mke wa Mtu
Erasto Raphaely Kabupa (50) mkazi wa kijiji cha Igelehedza kata ya Ilembula wilaya ya Wanging’ombe mkoani Njombe amedaiwa kufariki Dunia wakati akishiriki tendo la ndoa na mke wa mtu katika nyumba ya kulala wageni.
Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Njombe Mahamoud Banga amethibitisha taarifa za kifo hicho ambapo amesema mnamo June 8,2025 majira saa mbili usiku,Erasto (marehemu) alikuwa na mwanamke ambaye jina lake limehifadhiwa katika nyuma ya kulala wageni na wakati wakiendelea na tendo alizidiwa ghafla na kukimbizwa kituo cha afya Ilembula lakini alifikishwa akiwa tayari amepoteza maisha.
“Baada ya kufikishwa hospitali alitambulika amefariki dunia lakini awali alifika na mwanamke kwenye gesti inayoitwa Mwendavanu kwa lengo la kushiriki tendo la ndoa na kimsingi sisi hatuna taarifa kama alikuwa ametumia dawa hilo ni swala la kidaktari”amesema Kamanda Banga
RPC Banga amesema kutokana na aina ya tukio Jeshi la Polisi haliwezi kumkamata mwanamke aliye kuwa pamoja na marehemu huyo kwasababu wanaume wengi pia kwenye ndoa wamekuwa wakipoteza maisha kwasababu hiyo hivyo hawawezi kumkamata mtu kwa kufanya mauaji kwa tendo hilo.
Hata hivyo Diwani wa kata ya Ilembula Hezron Myale amesema kupitia taarifa ya familia ambayo imetolewa wakati wa mazishi yaliyofanyika leo katika kijiji cha Ilembula imebainisha kuwa sababu ya kifo cha Erasto Kabupa ni tatizo la moyo ambalo limekuwa likimsumbua kwa muda mrefu.
ALSO READ | Rais wa TFF Wallace Karia Ajiuzulu Rasmi….