Nature

Mbunge Mpina Ndani ya Kumi na Nane za Rais Samia “Hajalitendea Haki Jimbo Lake”

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amemkosoa Mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina, akimtaka aache tabia ya “kuruka ruka” na badala yake afanye kazi ya kuwatumikia wananchi wa jimbo lake.

Akihutubia mkutano wa hadhara uliofanyika Wilayani Meatu, Mkoani Simiyu, Rais Samia alisema Mbunge Mpina ameshindwa kuwatetea wananchi wa Kisesa ipasavyo bungeni na badala yake anataka ajitafutie umaarufu wa kisiasa. Alifafanua kuwa miradi ya maendeleo imetekelezwa Kisesa, lakini Mbunge huyo amechagua kupuuza hilo.

“Ndugu zangu maombi kama haya kuyaleta hapa kwenye mkutano kwa Rais, ni kujitafutia umaarufu na kuthibitisha kwamba Mbunge hakulifanyia haki jimbo lake. Angeasema bungeni kazi hii ingefanyika, kwa sifa alizozitoa na maelezo aliyoyatoa. SGR, Mwalimu Nyerere, Daraja la Busisi, MV Mwanza — huyu si Mbunge wa jimbo bali wa Taifa, kwahiyo nadhani tunapokwenda huko muache nimchukue kwenye nafasi zangu kumi.

Related Posts

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *