Dada wa marehemu Emmanuel Mathias maafuru CM PILIPILI, Veronica Mathias akizungumza na vyombo vya habari amesema kaka yake amefariki kwa maumivu makali na mwili wake umekutwa na majeraha na wao kama familia hawajui alipokuja Dodoma(jana) kutoka Dar Es Salaam hawakujua amefikia wapi.
Veronica amesema kuwa “Wakati anakuja na mahali alipofikia tulikuwa hatujui japo tulisikia anakuja Dodoma lakini habari za kujua ya kwamba hiyo harusi aliyokuwa anasherehesha inafanyikia wapi na yeye atafikia wapi hata hatukuweza kujua” Veronica Mathias – Dada wa Marehemu MC PILIPILI

