Mchezo wa Taifa Stars na Morocco Wafutwa

Mchezo wa Taifa Stars na Morocco Wafutwa
Mchezo wa Taifa Stars na Morocco Wafutwa

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limesema mchezo wa kirafiki wa kalenda ya FIFA kati ya Taifa Stars na Morocco uliokuwa umepangwa kuchezwa Oktoba 5, 2026 nchini Morocco umefutwa.

Uamuzi huo umefikiwa baada ya ripoti ya madaktari kubaini kuwa wachezaji watano wa Taifa Stars wamepata majeraha na hivyo hawataweza kushiriki mchezo huo.

TFF imesema baada ya kushauriana na Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Miguel Gamondi, wamekubaliana kuufuta mchezo huo.

Taifa Stars ilisafiri na wachezaji 23 pekee kwa ajili ya mchezo wa kufuzu AFCON 2027 dhidi ya Madagascar, kabla ya kutakiwa kucheza mchezo huo wa kirafiki.

Related Posts