Nature
MKUTANO wa Kutangaza Wagombea CCM Wasogezwa Hadi Saa 4 Leo Asubuhi

MKUTANO wa Kutangaza Wagombea CCM Wasogezwa Hadi Saa 4 Leo Asubuhi

Hadi muda huu saa kumi alfajiri, Mkutano wa Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama cha Mapinduzi CCM CPA. Amos Makalla na Wanahabari kwaajili ya kutangaza majina yaliyopita kwenye mchujo wa Kamati Kuu kupitisha majina ya wagombea ubunge watakaokwenda kupigiwa kura za maoni, haujafanikiwa kufanyika licha ya kusubiri kwa muda mrefu.

Wakati waandishi wa Habari wakiendelea kusubiri, wametaarifiwa kuwa kutokana na uzito wa mchakato ambao hadi sasa haujakamilika hivyo inalazimika Mkutano huo kufanyika Saa 4 Asubuhi.

Related Posts