Muuaji AJulikana Miaka 44 Baadae Kisa Sigara

Muuaji AJulikana Miaka 44 Baadae Kisa Sigara
Muuaji AJulikana Miaka 44 Baadae Kisa Sigara

Zaidi ya miaka karibu 44 baada ya Sarah Geer kubakwa na kuuawa akiwa na umri wa miaka 13, Mamlaka za California Nchini Marekani zimefanikiwa kumtambua Muuaji kupitia DNA iliyopatikana kwenye sigara ambayo iliyotupwa eneo la tukio ambayo kutokana na uwezo mdogo wa sayansi ya uchunguzi wa vinasaba (DNA) wakati huo, hakuna Mtuhumiwa aliyetambuliwa hivyo kesi hiyo iliwekwa kapuni.

Baada ya ushahidi huo wa sigara kuhifadhiwa kwa miaka, hatimaye teknolojia ya kisasa ya uchunguzi wa vinasaba (DNA) imewezesha kufanyika kwa uchambuzi wa kina uliowezesha Muuaji kujulikana kutokana na sigara hiyo kuchukuliwa eneo la tukio mwaka 1982 ambapo Mamlaka zinasema mafanikio haya yanaonyesha umuhimu wa kuhifadhi ushahidi na namna teknolojia inavyoweza kubadilisha mwelekeo na kwamba haki hata ikichelewa bado inaweza kupatikana.

Sasa Jopo la Majaji limempata na hatia James Unick – 64 (anayeonekana kwenye picha ya tatu ) akidaiwa kumuua Sarah ambaye sasa angekuwa na umri wa miaka 57.

Unaambiwa teknolojia ya “genetic genealogy inayochanganya ushahidi wa DNA na utafiti wa ukoo wa kifamilia, ilitumika kufanikisha uchunguzi huo ambapo DNA ya Unick iliyopatikana kwenye kipande cha sigara ililinganishwa na DNA iliyokuwa imehifadhiwa kwenye mavazi ya Sarah ambapo hatua hii imeelezwa kama ushindi mkubwa wa sayansi ya kisasa katika kusaidia mfumo wa hak

Related Posts