Mwamuzi Aliyekataa GOLI la Simba Dhidi ya Yanga Afungiwa Miezi Sita

Mwamuzi Aliyekataa GOLI la Simba Dhidi ya Yanga Afungiwa Miezi Sita
Mwamuzi Aliyekataa GOLI la Simba Dhidi ya Yanga Afungiwa Miezi Sita

Mwamuzi msaidizi namba moja (1) wa mchezo tajwa hapo juu, Kassim Mpanga kutoka Dar es Salaam, amefungiwa miezi sita (6) kwa kosa la kushindwa kutafsiri vema sheria za mpira wa miguu ambapo katika dakika ya 70 ya mchezo alikataa bao halali la klabu ya Simba kwa kile alichoonesha kwamba kulikuwa na kosa la kuotea kabla ya kufungwa kwa bao hilo.
Hata hivyo, taarifa ya wataalam wa kutafsiri sheria za mpira wa miguu, baada ya kufanyia tathmini video ya tukio hilo, imebainisha kwamba hakukuwa na kosa lolote kabla ya kufungwa kwa bao hilo.
Adhabu hii ni kwa mujibu wa Kanuni ya 42:1(1.8) ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti kwa Waamuzi.

Related Posts